Kufanikisha: Mwongozo wa kuwasaidia waumini kufanya shughuli zinazohusu VVU na UKIMWI - Tumeitwa Kuhudumia 2 (Paperback)
  • Kufanikisha: Mwongozo wa kuwasaidia waumini kufanya shughuli zinazohusu VVU na UKIMWI - Tumeitwa Kuhudumia 2 (Paperback)

Kufanikisha: Mwongozo wa kuwasaidia waumini kufanya shughuli zinazohusu VVU na UKIMWI - Tumeitwa Kuhudumia 2 (Paperback)

, , , , ,
£2.40
Paperback Published: 01/03/2009
  • Can be ordered from our supplier

Delivered within 3 weeks

  • This item has been added to your basket

Check Marketplace availability

Kitabu kidogo cha mwongozo wa kuwasaidia viongozi wa dini kuanzisha na kutekeleza miradi inayohusu VVU. Kina vipengele kuhusu kupanga mipango, kufanya maamuzi, kuandika mchanganuo wa mradi, kutayarisha bajeti, kuandika na kutoa taarifa ya mahesabu ya fedha, na kufanya ufuatiliaji na tathmini. Kitini cha TUMEITWA KUHUDUMIA kinajumuisha matendo, vijitabu vyenye kuhusisha matendo na miongozo midogo kuhusu mambo yanayohusu VVU na UKIMWI, vilivyoandaliwa kwa matumizi ya viongozi wa kanisa, hasa kwa nchi zilizo Afrika chini ya Jangwa la Sahara. Madhumuni ya mambo yaliyomo ni kuwawezesha wachungaji, mapadre, watawa wa kike na wa kiume, walei viongozi wa kanisa na waumini wao pamoja na jamii ili waweze: - Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ya janga la VVU na wito wa Kikristo wa kuitikia kwa huruma. - Kushinda unyanyapaa, ukimya, ubaguzi, kukataa, woga na kukataa kubadilika, hali ambazo zinazuia kanisa na jamii katika kukabiliana na mambo yanayohusu VVU na UKIMWI kwa ukamilifu zaidi. - Kuwaongoza waumini wao na jamii katika mchakato wa kujifunza na kubadilika kutakakopelekea kwenye matendo na mienendo ya kikanisa ili kuwasaidia watu binafsi, familia na jamii ili kupunguza kuenea kwa VVU na kupunguza athari za janga la VVU. TUMEITWA KUHUDUMIA ni wazo la Wadhamini wa Mikakati ya Kuleta Matumaini, ambao wanatayarisha na kutoa vitabu na video vinavyohamasisha mbinu madhubuti na michakato ya kijamii ya kuhudumia, kusaidia na kuzuia VVU na UKIMWI katika nchi zinazoendelea duniani, hasa zilizoko Afrika chini ya Jangwa la Sahara. TUMEITWA KUHUDUMIA inatekelezwa kupitia mchakato wa kimataifa, shirikisho la muungano wa makanisa, na taasisi nyingine za kidini, miundo ya kimataifa ya makanisa, wachapishaji, wasambazaji na washika dau wengine.

Publisher: Strategies for Hope Trust
ISBN: 9781905746118

You may also be interested in...

Your review has been submitted successfully.

We would love to hear what you think of Waterstones. Why not review Waterstones on Trustpilot?


Review us on Trustpilot